Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuundwa kwa UNMEER ni fursa bora zaidi kudhibiti Ebola: UNMIL

Mkuu wa vikosi vya UNMIL Meja Jenerali Leonard Ngondi. (Picha: UN/Grace Kaneiya)

Kuundwa kwa UNMEER ni fursa bora zaidi kudhibiti Ebola: UNMIL

Wakati baraza kuu la Umoja wa Mataifa likikutana leo kujadili hali ya Ebola huko Afrika Magharibi, Kamanda Mkuu wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa nchini Liberia, Meja Jenerali Leonard Ngondi amesema sasa kuna matumaini ya kutokomeza Ebola nchini humo kutokana na kuundwa kwa ujumbe maalum wa kudhibiti ugonjwa huo, UNMEER.

Amesema hayo katika mahojiano maalum na Idhaa hii kando kwa vikao vya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa anavyohudhuria mjini New York.

(Sauti ya Meja Jenerali Ngondi)

Amesema wananchi nao sasa wametambua kuwa Ebola ipo tofauti na awali.

(Sauti ya Meja Jenerali Ngondi)

Mahojiano kamili na Meja Jenerali Ngondi yatapatikana kwenye tovuti yetu.