Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Al-Shabaab haiwezi tena kushindana na AMISOM: Jen. Ntigurirwa

Luteni Jenerali Silas Ntigurirwa - Picha ya AMISOM / Abdi Dagane

Al-Shabaab haiwezi tena kushindana na AMISOM: Jen. Ntigurirwa

Wakati makamanda wakuu wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa wanakutana mjini New York, Luteni Jenerali Silas Ntigurirwa, ambaye ni Kamanda Mkuu wa vikosi vya ujumbe wa Muungano wa Afrika nchini Somalia, AMISOM, ameieleza idhaa hii jinsi AMISOM inajitahidi kupambana na wanamgambo wa Al-Shabaab nchini humo.

Amesema tayari miji muhimu na bandari kadhaa zimeshakombolewa katika operesheni iliyoanza mwezi Agosti, AMISOM wakiwazidi nguvu Al-Shabaab:

(Sauti ya Jenerali Silas)

Amejieleza pia kuhusu ripoti zinazotuhumu baadhi ya wanajeshi wa AMISOM kutekeleza vitendo vya ubakaji dhidi ya raia wa Somalia.

(Sauti ya Jenerali Silas)