Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bei ya vyakula kuendelea kushuka: FAO

Bidhaa za nafaka.Picha ya FAO

Bei ya vyakula kuendelea kushuka: FAO

Ripoti ya Shirika la Chakula na Kilimo Duniani, FAO, imesema soko ya chakula ni imara zaidi na bei ya bidhaa nyingi za kilimo imekuwa ni ya chini zaidi kuliko miaka ya hivi karibuni.

Ripoti hiyo imesema mavuno maradufu na hifadhi kubwa ya chakula ni sababu muhimu zilizochangia kushuka kwa bei ya nafaka duniani.

Mathalani uzalishaji wa ngano duniani unatabiriwa kufikia rekodi mpya ya juu mwaka huu, huku uzalishaji wa mchele ukitarajiwa kupungua kwa kiasi kidogo, ingawa hifadhi kubwa inatosha kukidhi mahitaji ya matumizi inayokadiriwa kufikia zaidi ya theluti moja ya matumizi ya kipindi cha mwaka 2015/2016.

Halikadhalika ripoti hiyo ya FAO iliyotolewa Alhamisi imesema uzalishaji wa nafaka mwaka wa 2014 unatarajiwa kufikia zaidi ya tani Bilioni 2.5, hii ikiwa ni ongezeko la tani millioni 65 zaidi kuliko makadirio ya awali ya FAO ya mwezi wa Mei.

FAO inasema kufikia mwisho wa mwaka wa 2015, hifadhi ya nafaka itafikia kiwango chao juu zaidi kuwahi kufikiwa katika kipindi cha miaka 15.