Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Benki ya dunia yaahidi dola milioni 50 kusaidia shughuli za kujisafi Haiti

UN Photo/Logan Abassi
Harakati za kuwasilisha maji safi nchini Haiti.

Benki ya dunia yaahidi dola milioni 50 kusaidia shughuli za kujisafi Haiti

Siku chache kabla ya kufanyika kwa mkutano wa wahisani kuhusu Haiti, Rais wa Benki ya Dunia, Dkt. Jim Yong Kim ameahidi dola Milioni 50 kwa ajili ya kusaidia huduma za maji na kujisafi nchini humo. Taarifa zaidi na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Dkt. Kim akizungumza mjini Washington DC amewaomba wafadhili wengine zaidi duniani washirikiane ili kuimarisha upatikanaji wa maji safi na huduma za kujisafi nchini Haiti kuzuia magonjwa yaambukizwayo kwa njia ya maji machafu.

Takwimu zinaonyesha kuwa ni asilimia 38 tu ya wananchi wa Haiti ndio wanapata maji safi na salama.

Amesema magonjwa kama vile kipindupindu, ndio moja ya sababu ya kwanza ya vifo vya watoto nchini humo, hali ambayo inaweza kukabiliwa iwapo wafadhili watatoa mchango unaohitajika.