Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHAS yaanzisha safari mpya za ndege katika kudhibiti Ebola

Picha: WFP

UNHAS yaanzisha safari mpya za ndege katika kudhibiti Ebola

Ofisi ya huduma za safari za anga za kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, UNHAS imeanzisha safari mpya za anga kwenye maeneo yaliyoathirika zaidi na ugonjwa wa Ebola huko Afrika Magharibi ili kurahisisha usafirishaji haraka wa watoa huduma za afya kwenye maeneo yaliyoathiriwa na Ebola.

Huduma hizo zinaratibiwa na shirika la mpango wa chakula duniani, WFP na safari hizo mpya ni baina ya Accra makao makuu ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa ya kushughulkia dharura ya Ebola na Dakar, Freetown, Monrovia na Conakry.

Naibu Mkuu wa masuala ya anga wa WFP Eric Perdison anafafanua kuhusu safari hizo.

(Sauti ya Perdison)

“Hii siyo operesheni kwa ajili ya wagonjwa wa Ebola, bali ni kwa ajili ya wafanyakazi wa kibinadamu. Lakini tunapaswa kuhakikisha tunachukua tahadhari zote zinazohitajika ili kuhakikisha wanasafiri salama na wakati huo huo kuhakikisha hatuhatarishi maisha ya watu wengine na wafanyakazi wa ndege wanaotekeleza jukumu hilo.”