Ebola haijakwamisha huduma za posta: UPU

8 Oktoba 2014

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la posta duniani, UPU,  Bishar A. Hussein amesema huduma za usafirishaji barua na vifurushi kuelekea nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone zilizokumbwa na ugonjwa wa Ebola inaendelea kama kawaida.

Akizungumza mjini Berne, Uswisi kwenye makao makuu ya shirikahilo, Bwana Hussein amesema mpaka sasa hawajapata maelekezo yoyote au ushauri kutoka shirika la afya duniani, WHO wa kutoshirikiana na nchi hizo na kwamba safari za ndege zinaendeleakamakawaida.

(sauti ya Hussein)

“Barua zetu zinasafirishwa kwa ndege na ali mradi ndege zinakwenda maeneo hayo, tutaendelea kushirikiana nazo. Hatujapata tatizo lolote kubwa linalohusu Ebola kwa kuzingatia mfumo wetu wa mtandao  uwasilishaji barua. Tutaendeleza biashara yetu na nchi hizo labda tupate maagizo vinginevyo kutoka Umoja wa Mataifa.”

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter