Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kenyatta ahudhuria kikao cha hatma ya kesi yake ICC

Uhuru Muiga Kenyatta akihudhuria kikao kuhusu hatma ya kesi dhidi yake huko The Hague, Uholanzi, tarehe 08 Oktoba 2014. (Picha:@ICC-CPI)

Kenyatta ahudhuria kikao cha hatma ya kesi yake ICC

Kikao cha mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC huko The Hague cha kujadili hatma ya kesi dhidi ya Uhuru Kenyatta leo kimeingia siku ya pili na mwisho ambapo upande wa utetezi umekanusha madai dhidi yake. Taarifa kamili na Assumpta Massoi

(Taarifa ya Assumpta)

Jaji Kuniko Ozaki ambaye ndiye kiongozi wa jopo linalosikiliza madai dhidi ya Kenyatta akieleza kutambua uwepo wa mtuhumiwa na kumkaribisha..

Ndipo Jaji Ozaki akamueleza sababu ya kikao hicho.

(Sauti ya Ozaki)

“Kama mnavayofahamu jopo limepokea ombi la upande wa mashtaka la kusitisha kusikiliza kesi hii, na upande wa utetezi kwa niaba yako linataka mashtaka yatupiliwe mbali. Uamuzi wa kukidhi ombi lolote utakuwa na athari kubwa na ni kwa misingi hiyo, mahakama imetaka uwepo wewe binafsi katika kikao hiki.”

Pamoja na maelezo hayo, Jaji huyo kiongozi alielezea madai ya upande wa mashtaka kuwa serikali yaKenyainakwamisha utoaji ushahidi na hadhi ya urais ya mshtakiwa ni kikwazo, Kenyatta ambaye hakuzungumza chochote mahakamani alijibu kupitia wakili wake Stephen Kay.

(Sauti ya Stephen)

“Hakuna ushahidi wa kitendo chochote, au kutochukua hatua yoyote, kuwa amefanya au ameepuka kufanya tangu kipindi cha ombi la ushirikiano wetu hadi leo.”

Baada ya awamu ya asubuhi, Jaji Kuniko aliahirisha kikao hicho hadi saa Kumi na Moja jioni kwa saa za Geneva, Uswisi akieleza kuwa ndipo watatoa uamuzi mwishoni.