Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban Ki-moon alaani mauaji ya mlinda amani Mali

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Senegal, mchini Mali. Picha ya MINUSMA/Blagoje Grujic

Ban Ki-moon alaani mauaji ya mlinda amani Mali

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali mashambulizi Jumanne kwenye kambi ya ujumbe wa umoja huo wa kuweka utulivu nchini Mali, MINUSMA yaliyosababisha kifo cha mlinda amani mmoja kutoka Senegal.

Ban kupitia taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa pamoja na kulaani kitendo hicho amerudia wito wake wa wa kutaka suluhu ya kisiasa ya mzozo huu.

Amezikumbusha pande zote kuwa zinawajibika kujizuia kushambulia jeshi la Umoja wa Mataifa.

Jumla ya walinda amani 31 wameuawa na wengine 91 wamejeruhiwa tangu Julai 2013 nchini Mali.

Tayari wanachama wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wamemepeleka salamu za rambi rambi kwa familia ya mhanga na serikali ya Senegal, wakisisitiza kuwa mashambulizi hayo yanaweza kuwa uhalifu wa kivita.