La msingi si kukopa au la, muhimu unatumia vipi mkopo: Dkt. Likwelile

7 Oktoba 2014

Mwaka 2014 ukiwa unayoyoma, taasisi za fedha za kimataifa ambazo ni Benki ya dunia na shirika la fedha duniani, IMF nayo yanakuwa na mikutano yao ya mwaka huko Washington DC. Lengo la mikutano hiyo ni kutoa fursa ya mijadala baina ya taasisi hizo na nchi wanachama zikiwemo zile za Afrika. Je nini matarajio ya Afrika? Assumpta Massoi wa Idhaa hii alizungumza na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha ya Tanzania Dkt. Servacius Likwelile, mmoja wa washiriki wa mikutano hiyo ambaye pamoja na mambo mengine amezungumzia suala la kukopa na madeni ikiwemo Tanzania na fursa zilizopo barani Afrika. Hapa anaanza kwa kuelezea ushirikiano ambao Afrika inataka na taasisi hizo.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter