Matumaini yapo katika ulinzi wa Bayo-anuai

7 Oktoba 2014

Nchini Korea Kusini, viongozi wa dunia na wataalam wa mazingira wanakutana kwa ajili ya kutathmini hali ya bayo-anuai duniani.

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Mpango wa Mazingira UNEP, Achim Steiner, amesema bado uwekezaji unahitajika ili kufikisha malengo ya ulinzi wa bayo-anuai ifikapo mwaka 2020.

Hata hivyo, ameeleza, matatizo yaletwayo na mabadiliko ya tabianchi, kama mafuriko, ukame na mmomonyoko wa ardhi yamesabibisha watu wengi kutambua kiambatanisho kati ya maendeleo na ulinzi wa mazingira.

Kwa hiyo,amesema, kuna matumaini makubwa:

Hakuna njia mbadala ila kuwa na matumaini. Tukianza kukosa rajua, kwanza tutaondoa matumaini ya kizazi kijacho ya kufurahia vitu maridadi vinavyoletwa na mazingira. Na pili tutashindwa kufikisha ujumbe wetu. Hatufanyi bidii ya kutosha lakini tunaweza kujitajidi zaidi, tunapswa kutumia ujumbe huu wakati wa kukabiliana na changamoto za ulinzi na matumizi ya rasimali za bayo-anuai.”

Achim Steiner ametoa mfano wa mradi wa REDD unaofadhiliwa na Shirika la UNEP pamoja na Shirika la Chakula na Kilimo Duniani FAO na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP unaolenga kurejesha hali ya misitu na kupunguza gesi chafuzi angani kwa kupanda miti.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter