Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfumo mpya wa uwekezaji endeleveu watarajiwa kuzinduliwa Geneva

Dkt. Mukhisa Kituyi, Katibu Mtendaji wa UNCTAD. (Picha@UN/Jean-Marc Ferré)

Mfumo mpya wa uwekezaji endeleveu watarajiwa kuzinduliwa Geneva

Wakuu kadhaa wa mashirika ya kimataifa na wadau wengine wa sekta ya kibinafsi wanakutana mjini Geneva 13–16 October na wakuu wa nchi na mamlaka za serikali ili kuzindua jitihada kubwa mpya za uwekezaji kwa ajili ya maendeleo, katika mkutano wa uwekezaji wa dunia wa Kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu Biashara na Maendeleo, UNCTAD 2014.

Katibu mkuu wa UNCTAD, Mukhisa Kituyi amesema, kutokana na kukabiliwa na hali sawa ya kiuchumi duniani, changamoto za  kijamii na kimazingira, jumuiya ya kimataifa inabuni malengo ya maendeleo endelevu badala ya malengo ya maendeleo ya milenia wakati tarehe ya ukomo wa malengo hayo mwakani inapokaribia.

Kituyi amesema, sehemu muhimu ya malengo hayo mapya itakuwa mfumo imara wa ufadhili.

Mkutano huo wa kipekee utawaleta pamoja wawakilishi zaidi ya 2000 kutoka sekta ya kibinafsi na ya umma kutoka nchi zinazoendelea na zilizoendelea , na kutoa fursa ya kuzingatia sera na masharti ya uwekezaji katika ngazi ya kitaifa na kimataifa ili kushughulikia changamoto za maendeleo endelevu.