Huenda watu 97 wameambukizwa kirusi cha homa ya Marburg Uganda

7 Oktoba 2014

Wakati dunia ikiendelea kupambana na mlipuko wa Ebola huko Afrika Magharibi, kirusi kingine hatari cha Marburg kimezuka nchiniUganda katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Tayari mtu mmoja amefariki dunia, 37 wengine kuambukizwa huku 60 wakishukiwa kuambukizwa tangu kuzuka kwa ugonjwa huo mwishoni mwa mwezi jana, kama anavyoripoti John Kibego wa Radio washirika ya Spice FM nchini humo.

(Tarifa ya John Kibego)

Mhudumu mmoja wa afya amethibitishwa kuanga dunia baada ya kwambukizwa kirusi chaMarburgkatika wilaya ya katikati mwa nchi ya Mpigi.

Wahudumu wa afya wengine 60 wamaoshukiwa kwambukizwa wametengwa pamoja na wagonjwa 37 ili kuzuia mambukizi zaidi.

Mkurugenzi wa Huduma za Afyaa Dr. Jane Ruth Achan amethibitisha tarifa hii na kuwaomba wananchi kutoa tarifa kuhusu yeyote watakayemshuku kuwa na maradhi hayo.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa msaada wa kitaalamu na kifedha kusaidia katika juhudi dhidi ya janga hili kwa mujibu wa wizara ya afya.

Kirusi cha homa ya Marburg kina dalili zinazofanana na zile za Ebola kama vile kutapika damu na kuvuja kutoka tundu zote za mwili.

Ugonjwa huo uliwahi kulipuka hapa Uganda mwaka 2012 na kuua idadi ya watu tisa.

Mlipuko huu umetangazwa wakati harakati za kuwachuja wanaongia nchini zikiendelea ili kuzuia mambukizi ya kirusi cha Ebola ambacho kimesababisha vifo vya zaidi ya watu 40 katika nchi jirani ya Jamuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter