Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OHCHR yaelezea hali mbaya katika nchi za Afghanistan, Haiti , Syria

Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Maifa.(picha ya UM/maktaba)

OHCHR yaelezea hali mbaya katika nchi za Afghanistan, Haiti , Syria

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na haki za binadamu imefafanua hali jumla katika mataifa ya Syria,Afghanistan na Haiti huku ikielezea wasiwasi wake kuhusiana na kuongezeka kwa matukio ya kutisha katika mji wa Kobane ambao unaandamwa na wanamgambo wa IS.

Katika taarifayaomaofisa wa ofisi hiyo wamesema kuwa wamepokea taarifa juu ya kukwamua kwa mamia ya raia ambao wameshindwa kuvuka kwenda Uturuki ambako wangepata hifadhi.

Taarifa zaidi zinasema kuwa kiasi cha raia 10,000 wapo katika mazingira ya kuhatarisha kutokana na kushindwa kuvuka mpaka.

KuhusuAfghanistanofisi hiyo imeelezea masikitiko yake kuhusiana na adhabu ya kifo inayotarajiwa kutekelezwa kesho Jumatano.

Ofisi wa mwanasheria mkuu waAfghanistanimetangaza leo kwamba hukumu ya kunyongwa hadi kufa inayowakabili raia watano waliohusika na makosa ya wizi wa kutumia silaha na ubakaji itatekelezwa kesho.

Ikielezea kuhusuHaiti, ofisi hiyo ya Umoja wa Mataifa imezitolea mwito mamlaka za nchini hiyo kuanzisha uchunguzi wa haraka kuhusiana na kifo cha rais wa zamani wa taifahiloJean-Claude Duvalier  aliyeaga dunia siku ya Jumamosi.