Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sudan Kusini kuzindua kampeni kupinga utumikishaji wa kingono

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu kuhusu ukatili wa kingono katika vita, Zainab Hawa Bangura(Picha ya UM/maktaba)

Sudan Kusini kuzindua kampeni kupinga utumikishaji wa kingono

Sudan Kusini inajiandaa kuzindua rasmi kampeni ya kitaifa yenye lengo la kukabiliana na kutokomeza vitendo vya utumikishwaji wa kingono  ambavyo vinawaandama wasichana wengi nchini humo. Taarifa kamili na George Njogopa.

(Taarifa ya George)

Kampeni hiyo inayoendeshwa kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Jinsia, Watoto na Ustawi wa Jamii na mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa inatekelezwa nchini kote kwa kuhamasisha wananchi kuhusu athari ya vitendo hivyo.

Kampeni hiyo ambayo pia inaungwa mkono na mashirika ya kiraia imepangwa kuazna Oktoba 9 na kuendelea hadi Novemba 24 ikigusua maeneo yote ya taifahilo.

Kuanzishwa kwa kampeni hiyo kunatokana na mafanikio yaliyojitokeza mwaka uliopita wakati kulipoanzishwa kampenikamahiyo iliyopata uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa mashirika yote ya Umoja wa Mataifa yanayoendesha shughuli zake Sudan Kusini.

Katika kile kinachoelezwa ni kukaribisha ushiriki mpana zaidi vyombo mbalimbali vya habari pamoja na makundi ya watu wenye ushawishi wanashirikishwa kwenye kampeni hiyo iliyodhamiria kutokomeza kabisa vitendo vya kuwatumikisha wanawake kwenye vitendo vya ngono.

Kampeni hiyo imepigiwa chepuo na Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili wa kingono kwenye mizozo, Zainab Hawa Bangura aliyeko ziarani nchini Sudan Kusini ambaye amesema wanawake wengi ni wahanga.

(Sauti Bangura)

Natoa wito kwa wa Sudan Kusini kuchukua hatua  na kusema imetosha! ukatili wa kingono haupaswi kuvumiliwa nchini Sudan Kusini. Kwa wale ambao wamebakwa nasema, kilichofanyika sio kosa lako, hauko pekee yako, tafadhali nenda hospitali upate matibabu. Umoja wa Mataifa na wadau utafanya kila uwezalo kukusaidia. Kwa watu ambao wamefanya ukatili huo nasema, tutakusaka kwa njia yoyote ile hakuna pahali pa kujificha, iwapo unafanya, au kuamrisha au kuvumilia ukatili huo tutakusaka, tutakukamata na kukuadhibu.”