Wekeza kwa walimu, wekeza kwa mustakhbali: UNESCO

6 Oktoba 2014
Kauli mbiu ya siku ya walimu duniani tarehe Tano Oktoba ambayo huratibiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO ni wekeza kwa walimu wekeza katika mustakabali. UNESCO kupitia chapisholakekuhususiku ya walimu duniani inasema Ukosefu wa waalimu duniani husababisha nchi nyingi kuajiri walimu wasio na ujuzi au wenye ujuzi usiotosheleza jambo linalosababisha kushuka kwa kiwango cha elimu.

Mathalani chapisho hilo linatolea mfano nchi za Afrika zilizoko kusini mwa jangwa la Sahara ikisema zina upungufu mkubwa wa walimu  ambapo theluthi mbili ya walimu inahitajika ifikapo mwaka 2030.

Je nini mtazamo wa walimu kuhusu hoja hii ya wekeza kwa walimu, wekeza kwa mustakhbali? Tumepita hapa na pale huko Afrika Mashariki kupata maoniyao, tukianziaKenyaambako  Salim Chiro wa radio washirika Pwani Fm ya Mombasa amezungumza na baadhi yao.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter