Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Walimu wasikate tamaa, wajitahidi kufundisha: Mwalimu mstaafu Kabera

Mwalimu mstaafu Henry Stephen Kabera (Kushoto) katika mahojiano na Tamimu Adamu.(Picha:UN/hisani ya Tamimu Adamu)

Walimu wasikate tamaa, wajitahidi kufundisha: Mwalimu mstaafu Kabera

Henry Stephen Kabera ni mwalimu mstaafu nchini Tanzania ambaye alifundisha shule za sekondari ikiwemo ile ya wavulana ya Songea na akamalizia utumishi wa ke wa umma kwenye shule ya sekondari ya Ruvuma. Katika kuadhimisha siku ya walimu duniani inayoangazia kuwekeza kwa walimu ili kuimarisha mustakhbali wa baadaye, mwenzetu Tamimu Adamu wa Radio washirika Jogoo FM ya Ruvuma alikutana naye na kufanya naye mahojiano ili kupata uzoefu wake na mtazamo wake kuhusu ualimu kwenye zama za sasa. Je nini mtazamo wake? Basi ungana naye kwenye mahojiano haya ambapo Mwalimu mstaafu Kabera anaanza na historia ya kazi yake ya ualimu.