Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ashtushwa na mashambulizi dhidi ya walinda amani Mali

UN Photo.
Katibu mkuu Ban Ki-moon. Picha:

Ban ashtushwa na mashambulizi dhidi ya walinda amani Mali

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameeleza masikitiko yake kufuatia taarifa za kushambluliwa na kuuawa kwa walinda amani Tisa wa Umoja huo nchini Mali, MINUSMA, siku ya Ijumaa.

Msemaji wa Ban amemkariri Katibu Mkuu akisema mashambulizi hayo ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa akikumbusha vikundi vilivyojihami juu ya ahadi yao ya kushirikiana na Umoja kuzuia mashambulizi dhidi ya walinda amani.

Ahadi hiyo ni kwa mujibu wa azimio la tarehe 16 Septemba la mjini Algiers ambapo Katibu Mkuu amesema wakati mashauriano ya amani yanaendelea ni lazima pande zote zionyeshe nia njema na azma ya kusaka suluhu ya mzozo kwa njia ya amani.

Ban ametuma rambirambi kwa familia za wafiwa pamoja na serikali ya Niger ambako ndio askari waliouawa wanatoka huku akiwahakikishia wananchi wa Mali kuwa Umoja wa Mataifa uko na mshikamano nao katika kusaka amani.

Shambulio la Ijumaa lilitokea wakati msafara wa walinda amani hao ukisafiri kutoka Ménaka kuelekea Ansongo kwenye mkoa wa Gao.