Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dunia yatakiwa kushiriki matembezi ya kupinga kuuwawa kwa ndovu na faru

UN Photo/JC Mcllwaine
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Tanzania. Picha:

Dunia yatakiwa kushiriki matembezi ya kupinga kuuwawa kwa ndovu na faru

Tarehe nne oktoba  kutafanyika matembezi  sehemu mbalimbali duniani kwa ajili ya kupinga kuuwa kwa ndovu na vifaru kwa sababu za uwindaji haramu na ujangili.

Kwa mujibu wa shirika la mpango wa mazingira la  Umoja wa Mataifa UNEP, zaidi ya tembo 35,000 na zaidi ya vifaru 1000 huuwawa kila mwaka na hivyo kutoa wito kwa dunia kukomesha mauaji hayo ambayo huenda yakasababish kutoweka kwa wanyama hao.

Katika mahojiano na idhaa hii Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete amesema serikali ya Tanzania yenye hifadhi zenye ndovu na faru imechukua hatua mahususi.

(SAUTI KIKWETE)