Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku za kazi kwa wiki zisizidi Nne ili kuweka ufanisi: Mtalaam ILO

UN Photos/Kibae Park
Wafanyakazi nchini Bangladesh Picha ya

Siku za kazi kwa wiki zisizidi Nne ili kuweka ufanisi: Mtalaam ILO

Mtalaam wa Masuala ya Hali ya Kazi katika Shirika la Kazi Duniani ILO, Jon Messenger, ameshauri siku za kazi kwa wiki ziwe nne badala ya tano.

Messenger ametaja sababu ya kwanza kuwa ni saa nyingi za kazi zinaweza kusababisha maradhi mengi yakiwemo moyo, akili, mgongo na hata kifo.

Pili amesema saa chache za kazi zitapatia ajira wengine waliokosa kazi na tatu ni uhifadhi wa mazingira akisema kuwa siku nne badala ya tano kutapunguza safari za kwenda kazini na utoaji wa gesi chafuzi kwa asilimia 20.

Amesema kufanya kazi muda mfupi zaidi kunaleta uwiano kati ya maisha ya kazini na nyumbani, na kuepuka na migogoro ya nyumbani.

Mtaalamu huyo amesema utafiti unaonyesha ni vyema kufanya kazi kwa saa chache lakini kwa bidii zaidi kuliko kuwepo kazini kwa saa nyingi bila kuwa na ufanisi.

Kwa ujumla, amesema takwimu zinaonyesha kwamba wiki fupi ya kazi italeta raha zaidi kwenye maisha ya watu.