Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na ICC umeleta manufaa:

Ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na ICC umeleta manufaa:

Miaka kumi ya makubaliano ya ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC imekuwa na umuhimu katika jitihada za pamoja za jumuiya ya kimataifa za kuepusha watekelezaji wa uhalifu kukweka mkono wa sheria.

Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa ya pamoja ya Katibu Mkuu Ban Ki-Moon na Rais wa ICC Sang-Hyun SONG iliyotolewa katika kuadhimisha siku hiyo Ijumaa Oktoba Tatu.

Taarifa hiyo imesema makubaliano yaliyoanzisha ushiriano huo yalizingatia misingi ya imani ya pande mbili hizo kuwa amani inaweza kupatikana iwapo wahusika wa machungu yaw engine wanaweza kufikishwa mbele ya sheria.

Ban na Rais huyo wa ICC wamesema wamejizatiti kuimarisha ubia kati ya taasisi hizo mbili, ubia ambao wamesema ni muhimu kwa jamii thabiti ya kimataifa na ulinzi wa maslahi ya jamii.