Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yakaribisha kuachiliwa kwa watoto wa Kikurdi waliokuwa wametekwa

UNICEF yakaribisha kuachiliwa kwa watoto wa Kikurdi waliokuwa wametekwa

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF limekaribisha kuachiliwa kwa watoto 70 wa Kikurdi waliokuwa wametekwa kwa siku 120.Taarifa kamili na Abdullahi Boru.

(Taarifa ya Abdullahi)

Watoto hao walitekwa mnamo tarehe 29 Mei, 2014, walipokuwa wakisafiri kutoka mji wa Ai’n Al Arab ulioko kwenye jimbo la Allepo, kaskazini mwa nchi, wakienda kufanya mtihani wao wa mwisho shueleni.

Msemaji wa UNICEF Christophe Boulierac amesema kuwa hali ya afya ya kimwili na kisaikolojia ya watoto hao inatathminiwa kwa sasa, akiongeza kuwa bado wanahofia usalama wa watoto na walimu ambao bado wamo matekani.

“Hali ya kimwili na kisaikolojia ya watoto hao kwa sasa inatathminiwa. Bado tuna wasi wasi mkubwa kuhusiana na watoto na walimu walio matekani. Utekaji nyara, kuajiri na kuwatumia watoto katika uadui ni ukiukwaji mkubwa wa haki za mtoto. Katika wakati huu wa vita, ni wajibu wa pande zote husika kuhakikisha kuwa watoto nchini Syria hawadhuriwi na wanapewa nafasi salama ya upatikanaji wa elimu.”