Wanaojidai ni wanamgambo wa kiislamu wanapotosha uislamu: Mjadala

2 Oktoba 2014

Tarehe 30 Septemba mwaka 2014 katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kulifanyika kikao cha kamati ya Baraza la Usalama la Umoja huo kinachohusika na harakati za kutokomeza ugaidi.

Kikao hicho kilichoandaliwa kwa pamoja na kamati hiyo na Morocco, kililenga kupata uzoefu wa nchi hiyo ya kifalme katika kukabiliana na ugaidi. Mali na Guinea ambazo zimetajwa kunufaika na mfumo wa Morocco nazo zilizoa ushuhuda wao huku washiriki wakiangazia kile kilichoibuka cha baadhi ya vikundi vilivyojihami kujiita kuwa ni vikundi vya kiislamu.

Je ni yapi yalijiri? Basi kwa kupata muhtasari wake, ungana na Assumpta Massoi kwenye makala hii.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter