Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Machafuko yasababisha vifo vya wanafunzi zaidi ya mia moja Palestina: UNRWA

Shareef Sarhan/UNRWA Archives

Machafuko yasababisha vifo vya wanafunzi zaidi ya mia moja Palestina: UNRWA

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhifadhi wakimbizi wa Kipalestina UNRWA linasema machafuko katika ukanda huo yamesababisha vifo vya wanafunzi zaidi 130 tangu mwezi July, majeruhi zaidi ya 800 huku wanafunzi wengine zaidi ya 500 wakiachwa yatima.

UNRWA katika taarifa yake inasema kuwa licha ya wanafunzi zaidi ya 140,000 kurejea shuleni lakini machafuko yameacha majeraha mengi miongoni mwao ikiwamo kusambaratishwa kwa maisha, kuvunjika mioyo, na athari za kisaikolojia ambazo shirika hilo limeahidi kuzishughulikia.

Katika kusaidia saikilojia za wanafunzi UNRWA kupitia mpango wake wa afya ya akili katika jamii imetoa mafunzo kwa walimu juu ya namna ya kutoa misaada ya kisaikolojia. Mafunzo hayo yamehusisha namna ya kumudu msongo wa mawazo, stadi za msingi na shughuli za burudani.

Tathimin inaonyesha kuwa takribani nyumba za wakimbizi elfu 80,000 zimeharibiwa katika kipindi cha siku hamsini za machafuko kiwango ambacho ni kikubwa kuliko kile kilichotahiminiwa awali cha 60,000. Mjini Gaza wengi kati ya zaidi ya watu 100,000 waliokosa makazi ni watoto.