Uhalifu wa ISIS ni ukiukwaji wa haki za binadamu wa kushtusha

2 Oktoba 2014

Nchini Iraq, mashambulizi yanayotekelezwa na wanamgambo wa ISIL ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNAMI na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu. Taarifa zaidi na Joshua Mmali.

(Taarifa ya Joshua)

Ripoti hiyo inawashutumu wanamgambo wa ISIS kwa kutekeleza uhalifu mkubwa ukiwemo kulenga raia wa kawaida na vikundi ya watu walio wachache kama Wakristo, Wayazidi au Washi’a, kubaka na kuteka nyara, kutumikisha watoto jeshini na kuharibu sehemu za ibada.

Halikadhalika ripoti imetaja ukiukwaji wa haki za binadamu unaodaiwa kufanywa na jeshi la serikali la Iraq ikiwemo kurusha makombora bila kujali raia.

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu Zaad Reyd Al-Hussein amesema vitendo hivyo vinaweza kuwa uhalifu wa kivita au uhalifu wa kibinadamu.

Rupert colville ni msemaji wa Ofisi ya Haki za Binadamu.

(Sauti ya Rupert)

“ Kamishna mkuu wa haki za binaadamu, Zeid Ra’ad Al-Hussein, leo anatoa wito kwa serikali ya iraq kuwasilisha jambo hili mbele ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu, na pia anatoa kwa serikali hiyo kuchukua uamuzi wa baadaye wa kujiunga na mahakama hii na mkataba wa Roma ambao ndio ulioanzisha ICC”.

Bwana Reyd Al-Hussein amewanukuu maimamu walioiandikia barua ISIL ya kuwaonya kwamba vitendo vyao vikiwa ni kuua raia wa kawaida, kuwageuza watumwa au kuwalazimisha kujisilimu ni kinyume na masharti ya dini ya kiislamu.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter