Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki za wakimbizi zamulikwa Geneva

Wakimbizi wa DRC washuka boti iliowaleta nyumbani baada ya kuvuka mto Oubangui.Picha © UNHCR/G.Diasivi

Haki za wakimbizi zamulikwa Geneva

Haki za wakimbizi ni miongoni mwa mambo yakliyomulikwa katika Kikao cha Utendaji cha Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR mjini Geneva huku ikilezwa idadi ya wakimbizi mwaka huu ikivunja rekodi kwa kufika milioni 51.

Kikao hicho kilichohutubiwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kimewaleta pamoja wawakilishi wa nchi mbali mbali na wadau wa masuala ya kuhifadhi wakimbizi akiwamo mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika ofisi ya Umoja wa Mataifa balozi Modest Mero anaeleza nafasi ya mkutano huo kwa Afrika.

(SAUTI MERO)