Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban Ki-moon atoa wito kwa biashara ya kimataifa yenye usawa

UNOG
Katibu mkuu Ban akihutubia katika mkutano wa Shirika la Biashara Duniani, WTO.

Ban Ki-moon atoa wito kwa biashara ya kimataifa yenye usawa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon amehudhuria uzinduzi wa kongamano la Shirika la Biashara Duniani, WTO, mjini Geneva, Uswisi, akitoa wito kwa biashara yenye usawa na uwazi ili kusaidia nchi zinazoendelea kufikia maendeleo endelevu.

Ameomba juhudi zifanyike ili kurekebisha soko la kimataifa kwa kuondoa ruzuku kwa bidhaa zinazouzwa nje na ushuru wa forodha. Pia ametaka nchi zinazoendelea zipewe fursa ya kutotozwa ushuru na kutowekewa vikwazo katika kuuza bidhaa nje.

Ameonya pia kwamba biashara ya kimataifa isipodhibitiwa ipasavyo inaweza kuathiri mazingira, kupitia utoaji wa gesi chafuzi wakati wa uzalishaji na usafirishaji wa bidhaa. Hata hivyo amesema:

“ Biashara ya kimataifa ni sehemu muhimu ya juhudi za kutokomeza umaskini, kuhakikisha usalama wa chakula na kuendeleza ukuaji wa uchumi. Fursa ndogo kabisa ya biashara inaweza kuwa maradufu ya msaada. Ikiimarishwa vizuri, biashara ya kimataifa inaweza kuwa ufunguo wa maendeleo endelevu”