Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Liberia, FAO, WFP waanza kutathmini hali ya chakula

Picha: WFP/Merel van Egdom

Liberia, FAO, WFP waanza kutathmini hali ya chakula

Serikali ya Liberia kwa kushirikiana na mashirika ya Umoja wa Mataifa yameanza kutathmini hali ya chakula hasa katika maeneo ambayo yameathiriwa na mlipuko wa homa ya ebola.

Mpango huo ambao ni ushirikiano wa pamoja baina ya Wizara ya Chakula, Shirika la Chakula na Kilimo FAO na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP, unalengo la kupata picha halisi juu ya hali ya chakula na maisha kwa ujumla.

Wataalamu kutoka pande zote wanakusanya taarifa kufahamu namna tatozo la homa ya ebola ilivyoathiri hali ya upatikanaji w achakula na baadaye wataalamu hao wataweka mikakati ya pamoja.

Kwa mujibu wa afisa kutoka FAO, Jesse Yuan mwishoni mwa tathmini hiyo kutaandaliwa mpango maalumu ambao utafanikisha kukabiliana na tatizo lolote litalojitokeza.