Leo ni siku ya wazee duniani; bado wengi hawapati mafao baada ya kustaafu: ILO

1 Oktoba 2014

Ikiwa leo ni siku ya wazee duniani, takribani nusu ya wazee wenye stahili ya kupata mafao baada ya kustaafu, yaani pensheni,  bado hawapati huku zaidi ya asilima 50 wanaopata pensheni hiyo haiwezi kuwatosheleza, inasema ripoti ya shirika la kazi duniani ILO.

Ripoti inasema hali hii husababisha wengi kati ya wazee duniani kutokuwa na usalama wa kipato na hawana haki ya kustaafu na kujikuta wakilazimika kufanya kazi muda mrefu huku wakilipwa malipo duni na kuwa katika hali hatarishi.

Inasema katika miaka ya hivi karibuni inaonyesha kuwa nchi nyingi za kipato cha kati na chini zimeongeza pensheni kupitia mfumo wa makato na ule usio na makato. Nchi 178 zilihusika katika utafiti wa ripoti hii kwa kuangalia mifumo ya pensheni ambapo imebainika kuwa zaidi ya nchi 45 zimefikia asilimai 90 za kiwango kinachotakiwa na zadia ya nchi 20 katika nchi zinazoendela zimefanikiwa au kukaribia katika kiwango cha pensheni kimataifa.

Ripoti hiyo imesisistiza kuwa wazee wana haki ya kustaafu kwa utu, bila kutumbukia katika umasikini japo hilo limetajwa kama tatizo duniani kote.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter