Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vita dhidi ya ugaidi isioteshe zaidi mbegu ya chuki: Ban

Mkuu wa Masuala ya siasa ndani ya Umoja wa Mataifa, Jeffrey Feltman. (Picha:UN /Paulo Filgueiras)

Vita dhidi ya ugaidi isioteshe zaidi mbegu ya chuki: Ban

Katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika kikao cha kamati ya umoja huo cha kukabiliana na ugaidi ambapo Katibu Muu Ban Ki-Moon ametanabaisha kuwa harakati zozote za kudhibiti vitendo hivyo vizingatie haki za binadamu.

Hotuba ya Ban ilisomwa na mkuu wa masuala ya siasa ndani ya Umoja huo Jeffrey Feltman akimnukuu Katibu Mkuu akisema kuwa kinyume cha hivyo harakati hizo zitakuwa ni mbegu ya kuimarisha vitendo hivyo.

(Sauti ya Feltman)

“Ni lazima kuepuka hatua za kukabili ugaidi ambazo zitachochea tatizo, kwani juhudi zinapofanyika ambazo hazilengi wahusika na hatimaye jamii nzima kuhisi kuwa haki zao za kibinadamu zinakandamizwa kwa misingi ya vita dhdi ya ugaidi hiyo ni kinyume na maadili na haina maana.”

Ujumbe wake kwa jumuiya ya kimataifa ukataka juhudi zijikite zaidi kwenye chanzo ili kumaliza tatizo hilo.

(Sauti ya Feltman)

“Wakati jumuiya ya kimataifa ina kila haki ya kujilinda dhidi ya kitisho hiki kwa kutumia mbinu zote za kihalali, ni lazima izingatie umuhimu wa kutatua chanzo cha misimamo mikali inayozua mizozo, kama kweli tunataka hatimaye kupatia suluhu la kudumu tatizo hili.”

Katika kikao hicho kulikuwepo na watoa mada ambapo miongoni mwao alikuwa Thierno Amadou Omar Hass Diallo,Waziri wa mambo ya dini na masuala ya kuabudu kutokaMaliambaye amesema anashangazwasanana mwenendo wa baadhi ya wanaojiita waumini wa dini ya kiislamu.

(Sauti ya Waziri Diallo)

“Nchi kama yetu yenye historia ndefu ya dini ya kiislamu, haikuweza kuelewa kwa nini uislamu unaweza kutumika kuhalalisha kukata mikono, kumkata mwanamke mwenye ujauzito wa miezi sita, kubaka wanawake kwa jina la uislamu. Kwa hiyo, kutokana na dira yetu tunayochangia na Morrocco,yaani ile ya shule ya Imam Malik, Malikia, ambayo ni uislamu wenye ustahimilivu mkuu. Tulijiambia kuwa  sisi tuna Imani, ni waislamu, lakini uislamu tunaoshuhudia siyo uislamu wa ukweli, Ndio maana wananchi waliopo Kaskazini mwa Mali hawakuunga mkono uislamu wenye msimamo mkali.”