Mjadala mkuu wahitimishwa, mambo muhimu yamewasilishwa:Kutesa

30 Septemba 2014

Mjadala Mkuu wa mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa umefikia ukingoni adhuhuri ya Jumanne tarehe 30 Septemba mjini New York, ambapo Rais wa Baraza hilo, Sam Kutesa amesema ushiriki wa dhati wa viongozi wa nchi wanachama umedhihirisha vile ambavyo wanachama wanatilia umuhimu wa chombo hicho.

Akizungumza baada ya hotuba ya mwisho kutoka Cabo Verde, Bwana Kutesa alitoa muhtasari wa yale yaliyogusiwa na watoa hotuba ikiwemo wasiwasi wao kuhusu Ebola.

(Sauti ya Kutesa)

Kuenea kwa kasi kubwa kwa Ebola huko Afrika Magharibi kulipatiwa kipaumbele sana wakati wa mjadala ambapo wazungumzaji wengi wakitaka uratibu wa haraka wa hatua za kudhibiti mlipuko huo.”

Rais huyo wa Baraza kuu akasema mjadala mkuu ni muhimu sana katika uwepo wa Umoja wa Mataifa lakini akatoa pendekezo ili mjadala huo uwe na mantiki zaidi.

(Sauti ya Kutesa)

“Ningalipenda kupendekeza kuwa kwa siku zijazo tufikirie kuweka kikanuni idadi ya mikutano na matukio mengine yanayofanyika sambamba na mjadala mkuu ili kuweza kujikita zaidi kwenye mambo yanayodaliwa hapa kwenye Baraza Kuu.”

Kwa mujibu wa Kutesa, mjadala huo ulihutubiwa na marais na wakuu wan chi 117, makamu Rais watatu, Manaibu Waziri wakuu wanane, mawaziri 56, wawakilishi Saba wa ujumbe kwenye Umoja wa Mataifa, Mkuu wa nchi moja yenye hadhi ya uangalizi pamoja na mwangalizi mmoja.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter