Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wabunge kinzani Libya wakutanishwa na UNSMIL, nuru yaonekana

Bernadino Leon, Mkuu wa Ujumbe wa Mataifa nchini Libya UNSMIL,

Wabunge kinzani Libya wakutanishwa na UNSMIL, nuru yaonekana

Wajumbe wa baraza la wawakilishi la Libya na wabunge waliosusia vikao vyake, wamekutana Septemba 29 chini ya uratibu wa ujumbe wa umoja wa Mataifa nchini humo UNSMIL.

Mkutano umefanyika mjini Ghadames ambapo baada ya mashauriano, mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Libya, Bernardino Leon pamoja na wawakilishi wa pande mbili hizo walizungumza na waandishi wa habari wakisema ilikuwa ni siku muhimu kwa Libya.

Leon amesema wamekubaliano kuanza mchakato wa kisiasa na kushughulikia masuala yanayohusu hali ya Libya na kwamba mchakato huo utafanyika kwa njia ya amani huku wakitoa wa kusitisha mapigano kamili kote nchini.

Wamegusia hali ilivyo kwenye viwanja vya ndege wakikubaliana kupatia suluhu ikiwemo kujaribu kufungua viwanja vyote ili safari ziweze kuanza na hivyo kuondoa machungu kwa familia.

Halikadhalika, Leon ambaye pia ni mkuu wa UNSMIL amesema wajumbe wa baraza la wawakilishi walituma ujumbe wa wazi kwamba wanataka kutatua matatizo ya watu wa kawaida wa Libya, watu ambao wamesema wameteseka, hasa baada ya wiki kadhaa za mapigano.