Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahitaji yaongezeka kwa zaidi ya wakimbizi wa ndani 295,000 Ukraine - OCHA

Familia kutoka Ukraine baada ya kuwasili Kyiev kwa njia ya reli © UNHCR/I.Zimova

Mahitaji yaongezeka kwa zaidi ya wakimbizi wa ndani 295,000 Ukraine - OCHA

Ofisi ya Kuratibu masuala ya Kibinadamu na Misaada ya Dharura, OCHA, imesema kuwa sasa kuna zaidi ya wakimbizi wa ndani 295,000 nchiniUkraine, huku zaidi ya watu milioni 5 wakiwa wanaishi katika maeneo yaliyoathiriwa na mapigano.

OCHA imesema mahitaji ya kibinadamu katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi yemeripotiwa kuwa makubwa mno, huku mashirika ya kitaifa ya kujitolea na Shirika la Msalaba Mwekundu yakiwa yamebakisha vifaa vichache tu vya misaada, na misaada michachesanakusambazwa kwa sababu za kiusalama.

Ofisi hiyo pia imesema kuna uhaba wa nguo za msimu wa baridi, vyatu, dawa, chakula na vifaa vya kujisafi ambavyo ni vigumusanakupatikana, huku baadhi maeneo ya makazi mashariki mwa nchi yakiwa na uhaba wa majisafiya kunywa.