Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kupunguza chumvi katika mlo kutaokoa maisha:WHO

Mamlaka Kuwait wanahimiza upunguzaji wa chumvi kwenye mikate.Nawal Al Hamad/WHO

Kupunguza chumvi katika mlo kutaokoa maisha:WHO

Wataalamu wa afya wanasema kwamba matumizi ya kupindukia ya chumvi yanaongeza shinikizo la damu na kuchangia kusababisha matatizo ya moyo.

Kwa wastani, watu hutumia karibu gramu 10 ya chumvi kwa siku, hii ikiwa ni karibu mara mbili ya pendekezo la WHO.

Ikiwa leo ni siku ya Moyo Duniani, Dk Temo Waqanivalu, mtaalam wa WHO kuhusu magonjwa yasiyoambukizwa amesema,

Ushahidi tulioona unaonyesha dhahiri kwamba utumiaji wa kupindukia wa chumvi, au madini ya Sodium unaongeza shinikizo la damu kwa watoto na watu wazima, na pia inaongeza hatari ya kuongezeka kwa magonjwa ya moyo, ikiwa ni pamoja na hususan kiharusi na ugonjwa wa moyo, kama mshtuko wa moyo”.