Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ISIS ni saratani inayopaswa kuondolewa: Netanyahu

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alipohutubia Baraza Kuu Septemba 29 2014 alitumia picha kama kielelezo cha watoto kutumika kama Kinga kwenye mzozo wa Gaza. (Picha:UN /Amanda Voisard)

ISIS ni saratani inayopaswa kuondolewa: Netanyahu

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amehutubia mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York akisema kuwa wanamgambo wanaotaka kujenga dola la kiislamu huko Iraq na Syria ni sawa na saratani ambayo inapaswa kuondolewa haraka iwezekanavyo.

Amesema kikundi hicho cha ISIS pamoja na magaidi wengine kwingineko duniani wenye misimamo mikali kuanzia Mashariki ya Kati, Afrika hadiAsiawameanza kujitanua kidogo kidogo na kuweka mazingira ya hofu siyo tu kwa wakristu na makundi madogo hata kwa waislamu wenzao.

(Sauti ya Netanyahu)

Uislamu wenye msimamo mkali unazidi kupanuka. Na huu sio uwanamgambo, wala siyo uislamu bali ni wanamgambo wenye msimamo mkali! Na cha ajabu, wahanga wao wa kwanza ni waislamu na hakuna aliye salamu. Sasa hiki kitisho kinaweza kuonekana kimeongezwa chumvi kwa baadhi ya watu, kwa sababu kilianza kidogo kama saratani kwenye sehemu Fulani ya mwili. Lakini isipoangaliwa, saratani hiyo inakua kubwa na kutishia mwili mzima.”

Waziri Mkuu huyo wa Israel ametaka Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kupanua wigo wake wa kumulika ukiukwaji wa haki za binadamu ili kudhibiti vitendo hivyo.