Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Timu ya UNMEER yawasili Ghana kuanza kazi dhidi ya Ebola

WHO ikileta vifaa ziada binafsi vya ulinzi na kutengwa katika wodi ya wazazi katika China-Guinea Urafiki Hospital Conakry, Guinea. Picha: WHO / T. Jasarevic

Timu ya UNMEER yawasili Ghana kuanza kazi dhidi ya Ebola

Timu ya ujumbe mpya wa Umoja wa Mataifa wa kushughulikia dharura ya ugonjwa wa Ebola (UNMEER) wakiongozwa na mkuu wa ujumbe huo Anthony Banbury imewasili nchini Ghana kuanza kazi ya kuutokomeza ugonjwa huo ulioshika kasi Afrika magharibi.

Wakati timu hiyo ikiwasili huko Ghana hapa New York rais Jakaya Kikwete wa Tanzania ambaye amehudhuria kikao cha 69 cha baraza kuu la Umoja wa Mataifa amezungumzia umuhimu kwa kila nchi barani Afrika kujihami dhidi ya Ebola akitolea mfano nchini mwake.

(SAUTI KIKWETE)

Mahojiano kamili na rais Kikwete kuhusu tahadhari ya ugonjwa wa Ebola na masuala mwengine yatapatikana kwenye ukurasa wetu.