Heko Dkt. Ahmadzai kwa kuwa Rais mpya wa Afghanistan.:UNAMA

29 Septemba 2014

Umoja wa mataifa umetuma pongezi zake kwa Dk Mohammad Ashraf Ghani Ahmadzai kufuatia kuapishwa kwake kuwa Rais wa Afghanistan.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Ján KubiŠ ambaye alihudhuria tukio la kuapishwa, pamoja na kutoa pongezi amesisitiza ushirikiano wa ofisi yake na serikali ya umoja wa kitaifa nchini Afghanistan kwa ajili ya amani, utulivu na maendeleo.

KubiŠ ambaye pia ni Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa Afghanistan, UNAMA amempongeza pia Rais huyo na Afisa Mtendaji Mkuu, Dk Abdullah Abdullah, kwa ahadi zao za kufanya kazi pamoja ili kuwatumikia wananchi wote wa Afghanistan kupitia serikali ya umoja wa kitaifa akisema ni matarajio yake kuwa serikali itaundwa haraka.

Mkuu huyo wa UNAMA amesema viongozi hao wawili wanabeba matarajio ya taifa hilo na kwamba changamoto nyingi zinazokabili Afghanistan zinaweza kutatuliwa kwa njia ya umoja na uzalendo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter