Urusi yaahidi kusongesha juhudi za kumaliza mzozo Ukraine

27 Septemba 2014

Urusi inafanya kazi bega kwa bega na Ukraine pamoja na shirika la usalama na ushirikiano Ulaya  OSCE) kutafuta suluhu la mzozo mashariki mwa Ukraine.

Hiki ndicho alichokisema waziri wa mambo ya nje wa Urudi, Sergey Lavrov kwa baraza la usalama hii leo alipohutubia kikao hicho jumamosi.

Amesema mgogoro kati ya serikali na vikosi vyaa waasi ambao umesababisha maelfu ya raia kukosa makazi umesababishwa na kile alichokiita mapinduzi ya serikali.

Akatoa ushauri nini kifanyike

 (SAUTI LAVROV)

"Njia ya kutanzua mzozo umefunguliwa na mafanikio ya makubaliano ya kusitisha mapigano Kusini Mashariki mw aUkraine kwa juhudi za rais Poroshenko na  Putin. Kwa ushiriki wa uwakilishi wa Kiev, Donetsk na Lugansk pamoja na OSCE na Urusi, hatua za kuchukua zimekubaliwa kwa ajili ya utekelezaji wa makubakliano, ukijumuisha utengwaji wa pande zinazokinzana, uondolewaji wa silaha nzito za jeshi la Ukraine na kuunda usimamizi kupitia OSCE."

Bwana  Lavrov amesema Urusi imejiandaa kuendelea kukuza utulivu wa kisiasa kufuatia mzozo nchiniUkraine.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter