Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sasa wananchi wa CAR washike hatamu kwenye mchakato wa siasa: Rais Samba-Panza

Rais wa serikali ya mpito huko CAR, Catherine Samba-Panza akihutubia Baraza Kuu. (Picha:UN/Cia Pak)

Sasa wananchi wa CAR washike hatamu kwenye mchakato wa siasa: Rais Samba-Panza

Kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, Rais wa  serikali ya mpito ya nchi hiyo Catherine Samba-Panza amehutubia mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, siku ya Jumamosi akisema wakati umewadia kwa wananchi wake kupatiwa fursa ya kusongesha mbele nchi yao.

Amesema hilo linawezekana kwani hali ya kibinadamu CAR imeimarika kwani asilimia 81 ya wakimbizi wa ndani sasa wamerejea makwao.

Kwa mantiki hiyo Rais Samba-Panza amesema ni vyema mchakato wa amani ukajikita ndani ya nchi kwa kuwapatia wananchi fursa ya kuchambua hali halisi na kubadilishana mawazo juu ya mwelekeo wa hatma ya nchi yao. Mathalani amesema kusaidia pande zote kwenye mzozo kukaa meza ya pamoja na kuunda taifa lao.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Radio ya Umoja wa Mataifa baada ya kutoa hotuba hiyo, Rais Samba-Panza amesema..

(Sauti ya Rais Samba-Panza)

Tarehe 15 mwezi huu ujumbe wa Muungano wa Afrika MISCA ulibadilishwa na kuwa wa Umoja wa Mataifa, MINUSCA kama njia mojawapo ya kusaidia mchakato wa ujenzi wa amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.