Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kenya imejipanga dhidi ya ugaidi na athari za mabadiliko ya tabianchi: Kenyatta

UN Photo/Amanda Voisard
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.

Kenya imejipanga dhidi ya ugaidi na athari za mabadiliko ya tabianchi: Kenyatta

Mkutano wa 69 wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa unaendelea katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York ambapo viongozi kutoka nchi mbalimbali wanachama wa Umoja wa Mataifa wanahutubia baraza hilo wakielza jumuiya ya kimataifa mambo kadhaa yakiwemo ya maendeleo aghalabu utekelezaji wa malengo ya maendeo, masuala ya amani na usalama na mengineyo.

Miongoni mwa marais wanaohutubia baraza hili kwa mara ya kwanza tangu kuapishwa kwao ni rasi wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye katika mahojiano maalum na Joseph Msami wa idhaa hii ameelezea mikakati ya serikali yake katika kupambana na mabadiliko ya tabia nchi, ugaidi na kwa ujumla utatuzi wa mizozo barani Afrika.

Kwanza Msami ameanza kumuuliza Kenya inafanya nini katika kuilinda nchi dhidi ya athari za mabadiliko ya tabia nchi.