Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mambo mseto:mjadala mkuu tabianchi, jamii za asili vyamulikwaa

Wiki ya mkutano wa Baraza Kuu la 69.Picha ya UM/Idhaa ya kiswahili

Mambo mseto:mjadala mkuu tabianchi, jamii za asili vyamulikwaa

Kwa wiki nzima, Kikao cha 69 cha Baraza Kuu  la Umoja wa Mataifa, kimekuwa kinaendelea na mikutano yake hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Tangu wiki iliyopita, marais na viongozi wengine wamekuwa mjin New York, wakishiriki mikutano na matukio muhimu yanayohusiana na masuala ya kipaumbele na katika Umoja wa Mataifa- tokea kukabiliana na ukatili wa kijinsia, suala la haki za jamii za asili hadi mabadiliko ya tabianchi.

Katika makala hii, tunamulika matukio hayo na mjadala mkuu wa Baraza Kuu. Kwanza, tuungane na Priscilla Lecomte mitaani mjiniNew York, akishiriki maandamano ya kihistoria ya kupigia debe tabianchi.