Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Teknolojia ya nyuklia inaweza kuchangia pakubwa katika maendeleo Afrika- Profesa Mkilaha

UN Photo/H Arvidsson
Tume maalum ya Umoja wa Mataifa (UNSCOM) ikifanya ukaguzi kwa lengo la kutambua na kuharibu silaha za kemikali ya nyuklia na vifaa vya ballistiska kombora. Picha:

Teknolojia ya nyuklia inaweza kuchangia pakubwa katika maendeleo Afrika- Profesa Mkilaha

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kutokomeza silaha za nyuklia, Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki, IAEA, linabonga bongo juu ya matumizi salama ya nishati hiyo likimulika haja ya kupunguza miyonzi isiyo ya lazima kuwafikia wagonjwa pale teknolojia ya nyuklia inapotumiwa katika tiba.

Hayo yamejadiliwa kwenye Mkutano wa kila mwaka wa IAEA hukoViennaAustriaambapo kando yake kumefanyika vikao vya ushirikiano wa nchi za Afrika kuhusu teknolojia ya nyuklia, AFRA, ukimulika jinsi nchi za Afrika zinaweza kushirikiana katika matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia.

Profesa Iddi Mkilaha, Mkurugenzi Mkuu wa tume ya nguvu za atomikiTanzania, na pia mwenyekiti wa AFRA, amezungumza na idhaa hii na kutueleza jinsi ushirikiano huu unaweza kulifaa bara la Afrika.

(Sauti ya Profesa Mkilaha)