Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika si nchi moja bali ni bara moja lenye mataifa 54: Rais Kikwete

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania akihutubia mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa New York, Alhamisi. (Picha:UN/Kim Haughton)

Afrika si nchi moja bali ni bara moja lenye mataifa 54: Rais Kikwete

Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa umeendelea kwenye Makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambapo awali akihutubia kikao hicho Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amesema Afrika si nchi moja yenye majimbo 54 bali ni bara lenye mataifa 54.

Alitumia mfano huo wakati akizungumzia vile ambavyo mlipuko wa Ebola huko Liberia, Guinea na Sierra Leone umechukuliwa kuwa ni kwa bara zima na kufanya bara zima linyanyapaliwe kwani baadhi ya nchi zimesitisha safari za ndege kwenda nchi zisizo na mlipuko

Rais Kikwete alifafanua zaidi alipohojiwa na mwandishi wa Idhaa hii.

(Sauti ya Rais Kikwete)

Alizungumzia pia siri yaTanzaniakutimiza lengo la kupunguza vifo vya watoto wachanga.

(Sauti ya Rais Kikwete