Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zambia yatakiwa ilinde haki ya wabunge ya kukusanyika

Nembo ya IPU

Zambia yatakiwa ilinde haki ya wabunge ya kukusanyika

Ujumbe wa muungano wa mabunge duniani, IPU ulioko nchini Zambia kuchunguza matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya wabunge umeitaka serikali kuchukua hatua zaidi kulinda haki ya kundi hilo kukusanyika bila vikwazo vyovyote.

Uchunguzi wa jopohiloumejikita kwenye visa vinavyohusisha wabunge 20 wa upinzani nchiniZambiaambao yadaiwa kuwa walinyanyaswa na polisi na hata kunyimwa hakiyaoya kukusanyika huku wengine wakishikiliwa na polisi.

Rais wa kamati ya IPU kuhusu haki za binadamu za wabunge Juan Pablo Letelier, ambaye ndiye anaongoza jopohiloamesema wana hofu kubwa juu ya madai hayo akisema kuwa wanataka sheria ya utulivu wa umma, POA iliyopitwa na wakati ifanyiwe marekebisho.

Wamesema sheria hiyo inakwamisha uwezo wa wanasiasa kukusanyika na hata kuwapatia polisi mamlaka kubwa ya kuhusika na mikutano ya kisiasa.

Jopo limetaka polisi kuchukuliwa hatua pindi wanaposisitiza vibali kutoka kwa wanasiasa wanapotaka kufanya mikutanoyaoilhali hakuna kifungu kinachotaja sualahilokwenye sheria hiyo ya POA.

Halikadhalika wametaka serikali yaZambiaipatie suluhu haraka kesi zinazohusisha wabunge watatu wa upinzani Dora Siliya, Maxwell Mwale na Hastings Sililo.

Wabunge hao walizuiwa bungeni mwaka 2011 kwa tuhuma za rushwa na vitendo visivyo halali.