Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Malawi itaendeleza juhudi za kulinda amani Afrika: Mutharika

UN Photo/Kim Haughton
Rais wa Malawi Arthur Peter Mutharika.

Malawi itaendeleza juhudi za kulinda amani Afrika: Mutharika

Rais wa Malawi Peter Mutharika amekuwa miongoni mwa viongozi kutoka Afrika waliohutubia kikao cha 69 cha baraza kuu la Umoja wa Mataifa ambapo pamoja na mambo mengine amezungumzia usalama na amani katika ukanda wa kusini kwa Afrika pamoja na utekelzaji wa malengo ya milenia.

Kandoni mwa hotuba yake rais huyo ambaye amehutubia baraza hilo kwa mara ya kwanza tangu aapishwe kuwa rais amezungumza na idhaa hii na kusema nchi yake imekuwa ikijihusisha na ulinzi wa amani katika ukanda mzima na kwamba itaendelea kufanya hivyo kwa maslahi ya usalama wa ukanda huo.

(SAUTI MUTHARIKA)

"Malawi inahusika na ulinzi wa amani mfano katika DRC, kuna vikosi vyetu na Afrika Kusini, Tanzania na vikosi vyetu viutaendeela kuwepo. Malawi pia ni mwanachama wa muungano wa nchi tatu uinayojumuisha Sfrika Kusini , Namibia na Malawi."

Akizungumzia utekelezaji wa malengo ya milenia rais huyo amesema licha ya kufanikiwa katika mazuingira lakini lengo la pili la elimu kwa wote ni changmoto kubwa.

(SAUTI MUTHARIKA)

"Licha ya kwamba tulianzisha elimu ya msingi baada ya mfumo wa vyama vipya mwaka 1994 lakini tulipuuza ugawaji wa vitendea kazi. Tulifikiri tu kutakuwa na shule za kutosha, walimu na madaftari hakuna kilichopo kwa sasa. Tunahitahi rasilimali nyingi kujenga madarsa, shule za walimu, maabara, vitabu vya kusomea, vyoo, pamoja na mabweni hususani kwa wasichana."