Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Licha ya matumaini Somalia, safari bado ndefu: Nyanduga

UN Photo/Tobin Jones)
Kituo cha wakimbizi cha Hawa Abdi Somali. Picha:

Licha ya matumaini Somalia, safari bado ndefu: Nyanduga

Katika kikao cha 27 cha Baraza la Haki za Binadamu kinachoendelea mjini Geneva, Mtalaamu Huru kuhusu Haki za Binadamu nchini Somalia, Bahame Tom Nyanduga, ametoa ripoti yake ya kwanza, akisisitiza changamoto zinazoikumba nchi hiyo.

Amekaribisha juhudi zilizofanywa na serikali ya Somalia tangu ilipoundwa miaka miwili iliyopita, akisisitiza umuhimu wa kuheshimu haki za binadamu hata wakati wa kupambana na ugaidi. Ameelezea zaidi maoni yake akiongea na mwenzetu Patrick Maigua kutoka Redio ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva.