Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa walaani mauaji ya mwanaharakati na mwanasheria Sameera Salih Ali Al-Nuaimy nchini Iraq

Nikolay Mladenov@Picha/UNAMI

Umoja wa Mataifa walaani mauaji ya mwanaharakati na mwanasheria Sameera Salih Ali Al-Nuaimy nchini Iraq

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Nickolay Mladenov amelaani mauaji ya ya mwanaharakati mashuhuri na mwanasheria Sameera Salih Ali Al-Nuaimy akisema ni muendelezo wa uhalifu wa kughadhibisha unaofanywa kwa watu wa Iraq na wanamgambo wa wanaotaka kuunda dola la Kiislamu, ISIL.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Bwana Mledanov ametumna salamu zake za rambirambi kwa famili ya mwanaharakati huyo na maelfu ya waaathiriwa wa vitendo vya kikatili vinavyotekelezwa na ISIL

Amesema kwa kumtesa na kumuua mwanaharakati na mwanasheria huyo ambaye alikuwa akitetea haki za binadamu kwa wakazi wenza huko Mosul kundi hilo limeendelea kujenga chuki na kuendeleza kutokujali utu wa binadamu.