Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban achagiza juhudi za kuafikia malengo ya milenia, Yvonne Chaka chaka ampigia debe

UN Photo/Rick Bajornas)
Mwimbaji Yvone Chaka Chaka (left) na Katibu Ban Ki-moon.

Ban achagiza juhudi za kuafikia malengo ya milenia, Yvonne Chaka chaka ampigia debe

Akizugumza na viongozi 300 wa ulimwengu waliokusanyika wakati wa mkutano wa ngazi ya juu kuhusu Malengo ya Maendeleo ya Milenia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewahisi viongozi hao kuhitimisha kazi iliyobaki kuhusiana na malengo hayo.

Ban amesema Malengo ya Maendeleo ya Milenia yamekuwa juhudi kubwa za kihistoria katika kupambana  na umaskini.

Katibu Mkuu amesema maisha ya mamilioni ya watu kote duniani yameboreshwa kutokana na juhudi za pamoja - katika ngazi ya kimataifa, kikanda, kitaifa na serikali za mitaa - za kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia.

Aidha, Ban amesema, tayari juhudi zimesaidia kuzuia vifo milioni 3.3 kwa malaria na vifo milioni 22 kwa ugonjwa wa Kifua Kikuu, mafanikio mengine zaidi yakitarajiwa kuafikiwa kufikia mwishoni mwa mwaka 2015.

Katika mkutano huo, mwimbaji maarufu wa Afrika Kusini Yvonne Chaka Chaka ambaye ni Balozi Mwema wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF na kuhusu Malaria, amewaomba vongozi waungane na kuendelea na juhudi zao:

(Sauti ya Chaka Chaka)

Naona mwanga mwisho wa barabara. Nataka kusema siyo wakati wa kusimama. Tusipochukua hatua sasa tutahukumiwa na kizazi kijacho. Ahsante kwa ripoti nzuri lakini ninachosema, ripoti haziokoi maisha. Tunapaswa kushinda vita hivi. mabibi na mabwana, barabara bado inajengwa.”

Chaka Chaka amemaliza wito wake kwa wimbo….

Cut Chaka Chaka 2