Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baadhi ya wapiganaji wa Al Shabaab Somalia waanza kujisalimisha: Kay

UN Photo/Rick Bajornas)
Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu, Somalia Nicholas Kay(

Baadhi ya wapiganaji wa Al Shabaab Somalia waanza kujisalimisha: Kay

Nchini Somalia matumaini ya amani yamepigwa jeki, huku ikielezwa kwamba baadhi wa wapiganaji wa Al Shabaab tayari wameanza kujisalamisha  kufuatia kuuawa kwa kiongozi wa kundi la kigaidi.Taarifa kamili na Abdullahi Boru

(Taarifa ya Abdullahi )

Suala la ugaidi limejadiliwa kwa ngazi ya juu siku ya Jumatano katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, likipitishwa pia azimio la kupambana na tatizohilo. Taifa la Somalia ni mojawapo ya nchi ambazo zimehangaishwa na kundi la Kigaidi la Al Shabaab.

Katika mahojiano na idhaa hii, Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu, Somalia Nicholas Kay amesema kuuawa kwa kiongozi wa Al-Shabaab ni chachu ya kupatikana amani ya kudumu nchini, japo juhudi za kijeshi ni lazima ziendelee.

(Sauti ya Kay)

“Imetoa nafasi ambapo serikali imetangaza mara moja msamaha kwa askari wa Al-Shabaab, na baddhi yao wamechukua fursa hiyo. Na tunawasihi wengine watathmini msimamo wao. Kuna vituo ambapo wanaweza kupata usaidizi na mafunzo zaidi ili watekeleze wajibu muhimu katika jamii. Wakati huo huo, ni muhimu shinikizo la kijeshi dhidi yao liendelee.