Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yataka msisitizo wa kutotumia chumvi ya ziada

Nembo ya WHO.(Picha ya UM/maktaba)

WHO yataka msisitizo wa kutotumia chumvi ya ziada

Wakati dunia ikijiandaa kuadhimisha siku ya moyo hapo Septemba 29, Shirika la Afya Ulimwenguni WHO limetoa wito ikitaka kutekeleza mpango maalumu wa kuzuia matumizi ya chumvi.

Shirika hilo limesema kuwa wakati umefika sasa kwa nchi kutekeleza kwa vitendo mkakati wa kuzuia matumizi ya ziada ya chumvi ili kunusuru maisha ya watu kukumbwa na magonjwa ya moyo na kiharusi.

Magonjwa hayo yasiyo ya kuambukizwa yanatajwa kusababisha idadi kubwa ya vifo na kwamba hivyo vimeongezeka zaidi katika miaka ya hivi karibuni.

Ili kukabiliana na hali hiyo, WHO imekuwa ikishirikiana na nchi duniani ili kuhakikisha kwamba matumizi ya chumvi ya ziada yanapungua.

Kulingana na Dk Chestnov chumvi huchukua sehemu kubwa ya chakula cha binadamu na kwamba kitendo cha kuongeza chumvi kwenye vyakula vilivyoandaliwa na kinaongeza hatari zaidi kwa afya ya mlaji.