Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mizozo inadidimiza maendeleo Afrika, juhudi zahitajika:Kenyatta

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya akihutubia mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. (Picha:UN/Cia Pak)

Mizozo inadidimiza maendeleo Afrika, juhudi zahitajika:Kenyatta

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amehutubia mjadala wa wazi wa mkutano wa 69 wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa akiangazia masuala ya afya, uchumi na kijamii pamoja na mizozo barani Afrika.

Mathalani kuhusu afya amegusia Ebola akisema kuwa Kenya itarejesha safari za ndege huko Afrika Magharibi pindi tu mamlaka za afya duniani zilizotoa angalizo awali zitatoa hakikisho kuwa ni vyema kufanya hivyo.

Kuhusu mizozo amesema suala la Sudan Kusini ni la masikitiko makubwa na kwamba jamii ya kimataifa na viongozi wa nchi hiyo ni lazima wachukue hatua na mwandishi wetu alizungumza na Rais Kenyatta afafanue zaidi.

(Sauti ya Kenyatta)

Kadhalika kiongozi huyo amezungumzia vita dhidi ya ugaidi nchini Kenya.

(Sauti ya Kenyatta)